LIGI Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/15 inatarajia kuanza kutimua vumbi kuanzia Septemba 20,mwaka huu.
Jumla ya timu 14,ndizo zinashiriki ligi hiyo ambayo kwa kutumia viwa
nja 10,ambavyo ni kile cha Taifa kilichopo Dar es Salaam kinachotumiwa
na timu za Simba na Yanga na Chamazi Compelex,ambacho kinamilikiwa na
timu ya Azam na kinatumiwa pia na timu ya Maafande wa JKT Ruvu.
Viwanja vingine ni Kambarage kinachotumiwa na timu ngeni kwenye ligi
ya msimu huu Stand United,Nangwanda Sijaona kitakachotumiwa na Ndanda FC
ya Mtwara,Jamhuri Kinachotumiwa na Polisi Moro,Mkwakwani uliopo Tanga
ambao utatumiwa na timu za Coastal Union na Mgambo JKT.
Uwanja mwingine ambao utatumika katika ligi hiyo ni ule wa Sokoine
uliopo Mbeya ambao unatumiwa na timu za Mbeya City na Prisons na uwanja
wa Mabatini uliopo Mlandizi Pwani unaotumiwa na timu ya Ruvu Shooting.
Shirikisho la soka Tanzania TFF,hadi sasa bado halijatoa ratiba ya
kuanza kwa ligi hiyo ambayo imekuwa na ushindani mkubwa katika ukanda wa
Afrika Mashariki lakini karibu timu zote 14 kwa sasa zipo katika
maandalizi makali kujiandaa na ligi hiyo na kukamilisha zoezi la usajili
ambao mwisho wake ni Agosti 17.
Timu kama Azam,Yanga na Simba zimeonesha kupania ligi hiyo kutokana
na usajili zilioufanya timu hizo kwa kusajili wachezaji kutoka Ulaya na
Amerika ya Kusini.
Yanga ambayo itakuwa chini ya kocha Mbrazili Marcio
Maximo,imewasajili wachezaji wawili kutoka taifa hilo analotokea kocha
wao Geilson Santana Santos ‘Jaja’ na kiungo Andrey Coutinho wakati Azam
imesajili Ismail Diarra raia wa Mali na Leonel Saint-Preux raia wa Haiti
na Simba imemchukua Pierre Kwizera raia wa Burundi aliyekuwa akicheza
soka Ivory Coast na ipo kwenye mazungumzo na aul Kiongera wa KCB ya
Kenya.
Wadau wengi wa soka wanasubiri kuona ni timu gani kati ya hizo tatu
zenye uwezo mkubwa wa kifedha ambao usajili wake utakuwa na faida baada
ya kutumia mamilioni ya pesa kwa ajili ya kuviboresha vikosi vya timu
hizo ambazo zimekuwa na ushindani mkubwa katika kuwania taji la ubingwa
wa Tanzania bara.
Timu kama Mtibwa Sugar,Mbeya City iliyotoa upinzani mkubwa msimu
uliopita Kagera Sugar,Coastal Union na nyingine nane zilizo baki nazo
zimekuwa na maandalizi kambe kujiandaa na msimu huu unaotaraji kuanza
Septemba 20 kwa viboresha vikosi vyao lakini mara nyingi zimekuwa sawa
na wasindikizaji na nyingine kujikuta zikishuka daraja.
Yanga ndiyo bingwa wa Kihistoria wa Ligi ya Tanzania bara baada
kunyakua taji hilo mara 24,tangu ligi hiyo ilipoanzishwa mwaka
1965,wakati huo ikiitwa ligi ya taifa na baadaye ilibadilishwa ikaitwa
ligi daraja la kwanza ambapo mwaka 1997 ilibadilishwa tena jina na
kuitwa Ligi Kuu kufuatia chama cha soka cha wakati huo FAT,kupata
udhamini kutoka kampuni ya Tanzania Breweries (TBL),kupitia yao ya
Safari Lager na Simba wanafuatia kwa kunyakua ubingwa huo mara 18.
Klabu nyingine ambazo zimewahi kutwaa taji hilo ni Cosmopolitan
(1967), Mseto SC, (1975) Pan African (1982), Mtibwa Sugar (1999 na 2000)
Tukuyu Stars (1986) na Coastal Union (1988) na Azam 2013/14.