Friday, August 15, 2014

Phiri aanza kazi rasmi Simba.

Phiri aanza kazi rasmi Simba.

Phiri aanza kazi rasmi Simba. 

 

Hiyo inakuwa ni mara ya tatu kwa Phiri kurudi Tanzania kukinoa kikosi cha Simba
KOCHA mpya wa Simba Patrick Phiri anatarajia kuiongoza timu hiyo kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa 2014/2015,ambao unatarajia kuanza Septemba 20 Goal imefahamu.
Phiri raia wa Zambia aliyesaini mkataba wa miaka miwili wa kukinoa kikosi cha Simba anarudi kwa mara ya tatu kuifundisha timu hiyo baada ya kutimuliwa kwa kocha Mcroatia Zdravko Logarusic,kufuatia kipigo cha mabao 3-0,kutoka kwa Zesco ya Zambia.
“Nimefurahi kupata nafasi nyingine kuwa kocha wa Simba najua niheshima kubwa kwangu kwa sababu Simba ni timu kubwa Tanzania na siku zote mashabiki wake wanapenda kuona wanashinda mataji ni changamoto kwangu kutokana na ushindani uliopo kwa sasa lakini nitahakikisha natumia ujuzi nilionao kuwapa furaha,”alisema Phiri.
Hiyo inakuwa ni mara ya tatu kwa Phiri kurudi Tanzania kukinoa kikosi cha Simba lakini ni mara ya pili kwa uongozi mpya uliopo chini ya Rais Evanse Aveva ambaye wiki tatu zilizopita alimpa mkataba wa mwaka mmoja kocha Logarusic kabla ya kumtimu Jumapili iliyopita.

Kukamilika kwa usajili wa beki huyo kunaifanya Yanga kufikisha idadi ya wachezaji watano iliyowasajili msimu huu

Kukamilika kwa usajili wa beki huyo kunaifanya Yanga kufikisha idadi ya wachezaji watano iliyowasajili msimu huu
Yanga yamnasa Edward Charles wa JKT Ruvu.
KLABU ya Yanga imefanikiwa kumpa mkataba wa miaka mitatu beki,Edward Charles,aliyekuwa akiichezea timu ya JKT Ruvu huku zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya dirisha la usajili kufungwa..

Dirisha la usajili linatarajia kufungwa Agosti 17 2014/15,na usajili huo unamaliza harakati za wapinzani wa Yanga,Simba waliokuwa wakiifukuzia saini ya mchezaji huyo anayemudu beki wa kushoto.
Goal inafahamu beki huyo tayari ameanza maisha mapya akiwa na miamba hiyo ya zamani ya Tanzania bara wanaonolewa na Mbrazili Marcio Maximo na sasa anajianda kuwania namba na mkongwe Oscar Joshua.
Kukamilika kwa usajili wa beki huyo kunaifanya Yanga kufikisha idadi ya wachezaji watano iliyowasajili msimu huu ambao ni Geilson Santana Santos ‘Jaja’Andrey Coutinho kutoka Brazili,wengine ni Pato Ngonyani,Said Juma na Charles

Yanga ndiyo bingwa wa Kihistoria wa Ligi ya Tanzania bara baada kunyakua taji hilo mara 24,tangu ligi hiyo ilipoanzishwa mwaka 1965,wakati huo ikiitwa ligi ya taifa


LIGI Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/15 inatarajia kuanza kutimua vumbi kuanzia Septemba 20,mwaka huu.
Jumla ya timu 14,ndizo zinashiriki ligi hiyo ambayo kwa kutumia viwa nja 10,ambavyo ni kile cha Taifa kilichopo Dar es Salaam kinachotumiwa na timu za Simba na Yanga na Chamazi Compelex,ambacho kinamilikiwa na timu ya Azam na kinatumiwa pia na timu ya Maafande wa JKT Ruvu.
Viwanja vingine ni Kambarage kinachotumiwa na timu ngeni kwenye ligi ya msimu huu Stand United,Nangwanda Sijaona kitakachotumiwa na Ndanda FC ya Mtwara,Jamhuri Kinachotumiwa na Polisi Moro,Mkwakwani uliopo Tanga ambao utatumiwa na timu za Coastal Union na Mgambo JKT.
Uwanja mwingine ambao utatumika katika ligi hiyo ni ule wa Sokoine uliopo Mbeya ambao unatumiwa na timu za Mbeya City na Prisons na uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi Pwani unaotumiwa na timu ya Ruvu Shooting.
Shirikisho la soka Tanzania TFF,hadi sasa bado halijatoa ratiba ya kuanza kwa ligi hiyo ambayo imekuwa na ushindani mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki lakini karibu timu zote 14 kwa sasa zipo katika maandalizi makali kujiandaa na ligi hiyo na kukamilisha zoezi la usajili ambao mwisho wake ni Agosti 17.
Timu kama Azam,Yanga na Simba zimeonesha kupania ligi hiyo kutokana na usajili zilioufanya timu hizo kwa kusajili wachezaji kutoka Ulaya na Amerika ya Kusini.
Yanga ambayo itakuwa chini ya kocha Mbrazili Marcio Maximo,imewasajili wachezaji wawili kutoka taifa hilo analotokea kocha wao Geilson Santana Santos ‘Jaja’ na kiungo Andrey Coutinho wakati Azam imesajili Ismail Diarra raia wa Mali na Leonel Saint-Preux raia wa Haiti na Simba imemchukua Pierre Kwizera raia wa Burundi aliyekuwa akicheza soka Ivory Coast na ipo kwenye mazungumzo na aul Kiongera wa KCB ya Kenya.
Wadau wengi wa soka wanasubiri kuona ni timu gani kati ya hizo tatu zenye uwezo mkubwa wa kifedha ambao usajili wake utakuwa na faida baada ya kutumia mamilioni ya pesa kwa ajili ya kuviboresha vikosi vya timu hizo ambazo zimekuwa na ushindani mkubwa katika kuwania taji la ubingwa wa Tanzania bara.
Timu kama Mtibwa Sugar,Mbeya City iliyotoa upinzani mkubwa msimu uliopita Kagera Sugar,Coastal Union na nyingine nane zilizo baki nazo zimekuwa na maandalizi kambe kujiandaa na msimu huu unaotaraji kuanza Septemba 20 kwa viboresha vikosi vyao lakini mara nyingi zimekuwa sawa na wasindikizaji na nyingine kujikuta zikishuka daraja.
Yanga ndiyo bingwa wa Kihistoria wa Ligi ya Tanzania bara baada kunyakua taji hilo mara 24,tangu ligi hiyo ilipoanzishwa mwaka 1965,wakati huo ikiitwa ligi ya taifa na baadaye ilibadilishwa ikaitwa ligi daraja la kwanza ambapo mwaka 1997 ilibadilishwa tena jina na kuitwa Ligi Kuu kufuatia chama cha soka cha wakati huo FAT,kupata udhamini kutoka kampuni ya Tanzania Breweries (TBL),kupitia yao ya Safari Lager na Simba wanafuatia kwa kunyakua ubingwa huo mara 18.
Klabu nyingine ambazo zimewahi kutwaa taji hilo ni Cosmopolitan (1967), Mseto SC, (1975) Pan African (1982), Mtibwa Sugar (1999 na 2000) Tukuyu Stars (1986) na Coastal Union (1988) na Azam 2013/14.
Ligi kuu bara inaanza lini?

TUNAWAKARIBISHA MWAMBENJA MUSIC CENTER KWA KAZI BORA KABISA

TUNAWAKARIBISHA MWAMBENJA MUSIC CENTER KWA KAZI BORA KABISA