Thursday, September 20, 2012

Maandamano makubwa nchini India

Maandamano makubwa nchini India

 20 Septemba, 2012 - Saa 12:41 GMT

Serikali ya India inakabiliwa na mzozo wa kisiasa baada ya kuidhinisha mageuzi makubwa ya kiuchumi wiki iliyopita.
Vyama vya upinzani na vyama vya wafanyakazi vinaandamana hii leo kupinga kupandishwa kwa kiwango kikubwa cha bei ya mafuta na ufunguzi wa sekta ya biashara kwa masoko ya kigeni kama vile Wal- Mart na Tesco.
Waandalizi walisema wanatarajia mamilioni ya watu kushiriki katika maandamano hayo.
Wafanyakazi walizuia njia za reli katika majimbo ya Uttar Pradesh na Bihar huku shughuli zikisitishwa katika ngome za upinzani katika majimbo ya Calcutta na Bangalore .
Lakini waandamanaji hawakujitokeza kwa wingi katika miji ya Delhi na Mumbai.
Chama cha Congress kinaamini kuwa maandamano hayo ni shinikizo muhimu kwa mageuzi nchini humo ingawa wadadisi wanasema kuwa mageuzi hayo yatatishia maisha ya kawaida ya mamilioni ya watu katika sekta hiyo ambayo haina mpangilio.

Helikopta ya Syria yaanguka Damascus

Helikopta ya Syria yaanguka Damascus

 20 Septemba, 2012 - Saa 12:55 GMT
Televisheni ya taifa nchini Syria imeripoti kuanguka kwa helikopta ya kijeshi karibu na mji mkuu Damascus baada ya kugongana kidogo na ndege ya abiria ambayo iliweza kutua salama.
Inaarifiwa kuwa ndege ya abiria ilikuwa imewabeba watu miambili.
Taarifa hiyo inasema ndege ya abiria ilitua salama katika uwanja wa ndege wa Damascus.
Mapema, duru za upinzani zilidai kuwa waasi ndio waliidungua helikopta hiyo.
Serikali imekuwa ikitumia helikopta na ndege nyinginezo katika harakati zake dhidi ya waasi.
Mwezi jana wapiganaji wa upinzani walidai kuidungua helikopta nyingine ya serikali.

Taharuki nchini Kenya baada ya mauaji

Taharuki nchini Kenya baada ya mauaji

 20 Agosti, 2012 - Saa 04:37 GMT

Baadhi ya watu wamelazimika kutafuta hifadhi sokoni kwa kuhofia usalama wao.
Tana River, Kenya
Tana River, Kenya
Mauaji hayo yalitokea wakati watu wenye silaha kutoka jamii ya Pokomo waliposhambulia kijiji kimoja katika eneo la Reketa huku wakiteketeza makaazi ya watu.
Mmoja wa wale walioathiriwa ameelezea BBC kwamba walishambuliwa usiku, ''hata tumekimbia kutoka kijiji chetu sasa. Walikuja kwa kijiji cha Riketa, watu walikuwa wanalala hata hawana habari wakavamia akina mama, watoto wote wamekufa hapa hapa.''
Alisema shambulizi hilo limewashangaza kwa sababu hata wakati mifugo wao wameingia kwenye mashamba, kuna njia ya kufidia, ''sisi kawaida yetu, hiyo mifugo inashikwa kisha unalipishwa. Sio kukatakata mifugo au kumaliza wachungaji.''
Naibu kamanda wa polisi mjini Mombasa, Joseph Kitur amesema uchunguzi wa awali umebainisha kuwa shambulio hilo lilifanywa na watu kutoka jamii ya Pokomo.
Jamii za Pokomo na Orma zimekuwa zikizozania malisho na maji tangu mwezi uliopita lakini shambulizi hili ndilo mbaya zaidi kutokea kati yao.
Mwaka wa 2001, karibu watu 130 walifariki wakati mzozo kati ya jamii hizo mbili ulipozuka.
Jamii ya Pokomo ni wakulima na huwa inategemea sana mto wa Tana kwa shughuli zao.
Jamii ya Orma ni wafugaji.
Mauaji hayo yameleta kumbukumbu za ghasia za baada ya uchaguzi za mwaka wa 2007, ambapo watu 1,200 walifariki katika mapigano.

Mancini amkemea Kipa Joe Hart

Mancini amkemea Kipa Joe Hart

 19 Septemba, 2012 - Saa 11:35 GMT

Kocha wa Man City Roberto Mancini
Mkufunzi wa klabu ya Manchester City Roberto Mancini amemuonya kipa wake Joe Hart dhidi ya kushutumu wachezaji wake, akisisitiza kuwa yeye pekee ndiye jaji.
Manchester City waliongoza mara mbili wakati wa mechi yao ya kuwania kombe la klbau bingwa barani ulaya dhidi ya Real Madrid, lakini walifungwa dakika za mwisho na mechi hiyo kumalizika huku Real Madrid ikiibuka na ushindi wa mabao 3-2.
Hart alisema haiwezekani kwa klabu yoyote ambayo inaongoza kwa mabao 2-1 huku ikiwa imesalia dakika tano za mechi na kasha ipoteze mechi hiyo. '' ni lazima sisi wenyewe tujilaumu'' aliongeza Hart.
Lakini Mancini amejibu kwa kusema, licha ya kukubalina na kipa wake, yeye anapaswa kutekeleza wajibu wake. ''mimi naweza kushutumu wachezaji wangu lakini sio Hart'' alisema Mancini.
Kabla ya mechi hiyo Manchester City ilikabiliwa na upinzani mkali kabla ya mchezaji wao wa ziada Edin Dzeko kufunga bao la kwanza kunako dakika ya 69.
Lakini Marcelo alizawazishia Real dakika saba kabla ya mechi kumalizika. Dakika mbili baadaya Aleksandar Kolarov aliifungia mabingwa hao wa England bao la la pili kupitia kwa mkwaju wa adhabu.
Karim Benzema na Cristiano Ronaldo walifunga bao moja kila mmoja dakika tatu za mwisho za mechi hiyo na kuisadia Real Madrid Kushinda kwa mabao 3-2.

Wachimba migodi warejea kazini

Wachimba migodi warejea kazini

 20 Septemba, 2012 - Saa 09:10 GMT

Wachimbaji wa Marikana

Wachimba migodi nchini Afrika Kusini wameanza kurejea kazini katika mgodi wa madini ya Platinum wa Marikana
Mgodi huo ulikuwa kitovu cha ghasia na mauaji ya wachimba migodi 44 waliozua ghasia wakati wakigoma kwa wiki sita kudai nyongeza ya mishahara .
Mapema wiki hii wachimba migodi waliafikia makubaliano ya asilimia 22 ya nyongeza ya mishahara ndipo wakakubali kurejea kazini.
Wamiliki wa mgodi wa Lonmin ambao ni wa tatu kwa ukubwa katika kuzalisha madini ya Platinum duniani, walielezea kupata hasara kubwa ya kifedha wakati mgodi huo ulipofungwa kufuatia mgomo wa wachimba migodi.
Jopo maalum limeundwa nchini humo kuchunguza vifo vya wachimba migodi waliouawa na polisi wakati wa migomo hiyo.

Mji wa Kismayo unakaribia kutekwa

Mji wa Kismayo unakaribia kutekwa

 20 Septemba, 2012 - Saa 09:45 GMT
Wanajeshi wa Kenya wakipambana na Al-Shabaab
Msemaji wa jeshi la Kenya Meja Emmanuel Chirchir anasema kuwa wanakaribia kuuteka mji wa bandarini wa Kismayo.
Meja Chirchir amekariri kuwa wapiganaji wa Kenya wanaopigania kundi la Al Shabaab ikiwa wataweza kujisalimisha watasamehewa
Kumekuwa na ripoti kuwa wapiganaji wa al-Shabaab wamenza kuutoroka mji huo katika siku chache zilizopita baada ya kuzingirwa na majeshi ya muungano wa Afrika kutoka pande zote
Mji huo ndio ngome ya mwisho ya Al-Shabaab, ambayo huitumia kwa kuingza silaha na zana za kivita kutoka nchi za kigeni.
Muungano wa Afrika unasema kuwa wanajeshi wa Somalia wameuteka mji wa Janaa Cabdlla ngome nyingine ya wapiganaji hao iliyo umbali wa kilomita hamsini Magharibi mwa Kismayo.

Makaburi ya Tana River yafukuliwa

Makaburi ya Tana River yafukuliwa

 20 Septemba, 2012 - Saa 10:50 GMT
Polisi wakilinda makaburi hayo ya siri
Polisi na wataalamu wa kuchunguza maiti wamepigwa na mshangao mkubwa baada ya kukosa kupata chochote ndani ya makaburi ya siri yaliyogunduliwa katika eneo la Tana River.
Polisi walipewa amri ya kufukua makaburi hayo hii leo katika kijiji cha Ozhi ambako mapigano kati ya jamii za Orma na Pokomo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu miamoja na kuwaacha maelfu bila makao.
Kwa mujibu wa naibu kamishna wa polisi eneo la Tana River, Anthony Kamitu, makaburi hayo yalikuwa na mitaro minne ishara kuwa watu walikuwa wamezikwa kwenye makaburi hayo.
Ingawa bwana Kamitu alisema kuwa hawakupata miili yoyote licha ya kuwa kulikuwepo na harufu mbaya ishara kwamba maiti waliokuwa ndani ya makaburi hayo waliondolewa.
Bwana Kamitu anasema kuna hofu kuwa wahalifu kutoka jamii ya Pokomo waliitoa hiyo miili kwenye makaburi hayo huku polisi wakisubiri kibali cha mahakama ili kuweza kuyafukua.
Polisi wamefahamisha BBC kuwa makaburi hayo yalikuwa tu na mguu mmoja wa kushoto wa mtu na wanashuku kuwa maiti waliokuwa ndani ya makaburi hayo waliondolewa na kupelekwa kwingineko.
Zaidi ya watu miamoja wamefariki katika mapigano kati ya jamii hizi mbili ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda wa mwezi mmoja ulipita.
Makabiliano kati ya jamii hizo mbili yalianza katikati ya mwezi jana na kusababisha mashambulizi ya kuvizia na ya kulipiza kisasi.

Tamko La Serikali Juu Ya Ghasia Za Uchaguzi Mdogo Bububu

Tamko La Serikali Juu Ya Ghasia Za Uchaguzi Mdogo Bububu


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema hakuna mtu aliyefariki kutokana na vurugu siku ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Bububu uliofanyika Jumapili iliyopita kama ililivyodaiwa. na gazeti moja linalotolewa kila wiki hapa nchini.

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Afisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar na kutiwa saini na waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed imeeleza hadi sasa hakuna taarifa yoyote ya kifo kilicho sababbishwa na vurugu hilo iliyoripotiwa.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa jeshi la Polisi lilipokea taarifa ya kujeruhiwa watu kutokana na vurugu za baadhi ya vitkundi vya wananchi vilivyojipanga kuwazuia wananchi wengine kwa makusudi kushiriki katika zoezi la kupiga kura.
Kuhusu tuhuma zilizo tolewa dhidi ya Makamo wa Pili wa Rais katika zoezi la upigaji kura taarifa hiyo ilieleza kuwa maelezo hayo siyo ya kweli na kwamba zinalenga kumchafulia jina Kiongozi huyo wa ngazi za juu

Kufuatia tuhuma hizo Serikali imemtaka Mharir wa Gazeti la FAHAMU kuthibitisha kwa maandishi tuhuma walizoandika dhidi ya Mheshimiwa Makamo wa Pili wa Rais au kumuomba radhi kwa maandishi kupitia Gazeti lake la FAHAMU katika kipindi kisichozidi siku saba(7) kuanzia tarehe ya taarifa hii. Vyenginevyo Serikali itachukuwa hatua zinazofaa dhidi ya wahisika wote.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kusikitishwa kwake na taarifa zilizotolewa na kiongozi mmoja wa Ngazi za juu wa CUF kupitia gazeti hilo kwa kumtaja Makamo wa Pili wa Rais kuwa kiongozi wa juu wa serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar aliyejitosa kuharibu matokeo ya kura kwa kuingia katika baadhi ya vituo kama kiongozi wa Wawananchi.

Tuhuma hizo si za kweli na zisingepaswa kutolewa na Kiongozi wa juu wa chama cha siasa kwani kiongozi huyo anaelewa fika kwamba tuhuma hizo zinachafua jina la kiongozi huyo na kuhatarisha Umoja wa Taifa Letu.

Kamati Ya Bunge Yapiga Marufuku Hoja Ya Majaji Kujadiliwa

Kamati Ya Bunge Yapiga Marufuku Hoja Ya Majaji Kujadiliwa


KAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE YATOA TAMKO UTEUZI WA MAJAJI WA MAHAKAMA KUU. 
 Na Veronica Kazimoto – MAELEZO Dar es Salaam 20/09/2012.
 Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imetoa tamko la kuwataka watendaji wa Serikali, Mahakama, vyombo vya habari na taasisi nyingine zote kuacha kuzungumzia suala la Uteuzi wa Majaji wa mahakama kuu kama lilivyowasilishwa Bungeni wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mwenyekiti wa kamati hiyo Brigedia Jenerali . Mstaafu Hassan Ngwilizi (Mb) amesema suala hilo liko mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ambayo inaendelea na uchunguzi hivyo haitarajiwi taasisi nyingine, nje ya Bunge kulizungumzia suala hili kwa kuwa linajadiliwa na Kamati ya Bunge. “Kamati imeamua kutoa tamko hili kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa uvunjifu wa kanuni na taratibu tulizojiwekea kwa mujibu wa Katiba na Sheria nyingine za nchi kutoendelea kuvunjwa”, amesema Ngwilizi. Ngwilizi amenukuu Ibara ya 100 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayosema kuwa kutakuwa na Uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu Katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, au katika mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge. “Uhuru wa utaratibu unaohifadhiwa na ibara hiyo ya Katiba umelipa Bunge mamlaka ya kujiwekea utaratibu wa kushughulikia masuala yake katika Kanuni za Kudumu za Bunge zilizotungwa chini ya Ibara ya 89 (1) ya Katiba”, amesisitiza Ngwilizi. Kutolewa kwa tamko hilo na kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kunatokana na mwongozo ulioombwa na Gosbert Blandes (Mb) wakati wa Hotuba ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani kwa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Tundu Lissu mbunge wa Singida Mashariki. Katika maelezo yake, Mhe. Blandes alinukuu ukurasa wa 9 aya ya 2 katika Hotuba hiyo iliyosomeka kuwa watu wanateuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ambao hawajawahi kupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama. Aya hiyo iliendelea kusema kuwa inaelekea watu hao hupewa ujaji kama zawadi ili kuwawezesha kupata mafao ya majaji wastaafu ambayo yameboreshwa na matokeao yake ni kuwa na majaji ambao wamechoka na hawawezi au hawajui namna ya kufanya kazi ya jaji wa mahakama kuu. Aidha Blandes alisema msemaji wa kambi ya upinzani ameingilia mhimili mwingine wa Mahakama ambao hauna nafasi ya kuja kujitetea ndani ya Bunge na maneno hayo yanalenga kuwadhalilisha Waheshimiwa Majaji kwamba hawana uwezo, wamechoka, na hawajui namna ya kufanya kazi. Kufuatia maneno hayo Mwenyekiti wa kikao hicho Jenista Mhagama (Mb), alitoa mwongozo wake kwa kuiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili ipitie mwenendo wa shughuli yote ya siku hiyo kama inavyoonekena katika taarifa rasmi za bunge (Hansard) na kulishauri Bunge zima kwa ujumla wake hatma ya kufanya katika jambo hilo.

We were frivolous in possession - Ferguson reflects on Manchester United's victory over Galatasaray

We were frivolous in possession - Ferguson reflects on Manchester United's victory over Galatasaray

The Red Devils boss criticized his side's performance after it edged to a slender win over the Turkish champion at Old Trafford, thanks to Michael Carrick's goal

By Nicholas McGee

\Sir Alex Ferguson bemoaned Manchester United's lack of composure after it scraped past Galatasaray in the opening game of its Champions League campaign.

A seventh-minute strike from Michael Carrick was enough to take all three points, but the Turkish champions had a number of chances to get back into the contest and Ferguson believes that the Red Devils were slightly fortunate to have come away from the game with the victory.

He told Sky Sports: "I think we expected a tough game, Galatasaray have got a lot of experience in their team and the first half we kept giving the ball away and they counter-attacked very well from that.

"It was a lack of concentration at times. It's unusual for us, it's unusual for us to be as frivolous on the ball as that. In the second half we did much better in that respect.

"I was happy with the second half, we were more solid, had better concentration and sorted out things really well."

Despite the slightly disappointing performance, the Scot was pleased to have witnessed his side take maximum points following a dismal campaign in the competition last term.

He added: "In the second half they never made any chances and all the chances fell to us, we could have scored four or five in the second half.

"We missed the chances we did in the second half, we kept ourselves on the edge really. I think to get the three points in the first game is a bonus really. If you go back to last season, we got a point at Benfica, so three points are really important."

'Nothing's hurting' - Kagawa emerges from Manchester United return fully fit The Japan international provided Michael Carrick the

'Nothing's hurting' - Kagawa emerges from Manchester United return fully fit

The Japan international provided Michael Carrick the game-winning assist as the hosts began their 2012-13 UEFA Champions League campaign with a win over Galatasaray.

By Dan Orlowitz

UEFA Champions League: Shinji Kagawa (Manchester United) - Selcuk Inan (Galatasaray)
getty
Manchester United attacker Shinji Kagawa insists he is fully fit after providing the game-winning assist in his team's 1-0 win over Galatasaray in their opening match of the UEFA Champions League group stage.

Kagawa made an impression in his first appearance since Sept. 6, where he was substituted at halftime in Japan's 1-0 friendly win against the United Arab Emirates.

After concerns over back pain that forced his withdrawal from Japan's World Cup qualifier against Iraq, the Samurai Blue star watched his club's 4-0 win last weekend against Wigan from the bench. He returned to start and play 84 minutes at Old Trafford on Wednesday.

"Nothing's hurting," Kagawa told Nikkan. "I've gotten back into form in practice, but I need to improve a bit more physically and increase my momentum."

Kagawa combined with teammate Michael Carrick in the eighth minute, sending the midfielder clear on goal with a well-placed pass from just outside the penalty area, one that Carrick slotted home for the lone tally.

"We got off to a good start at home," Kagawa said. "We had two or three chances to score, and then when we did convert it became an easier game to play.

"Once I got the ball, I was able to pick up speed and move toward the goal. That sort of play is important, but I'm disappointed that I wasn't able to take any big shots."

Neymar nets injury-time winner as Brazil defeats Argentina in Superclassico Das Americas

Neymar nets injury-time winner as Brazil defeats Argentina in Superclassico Das Americas

The Santos attacker helped the Selecao to victory with his goal well into stoppage time after previously providing the assist for the equalizer.

Friendly : Neymar, Brazil - China
Other
Brazil recorded a 2-1 victory over Argentina in the first leg of the Superclassico Das Americas in Goias on Wednesday.

Juan Manuel Martinez opened the scoring for the away side midway through the first half, but Paulinho restored parity shortly after. Neymar then decided the game well into stoppage time as he slotted home a penalty.

The hosts started the match the better side of the two, yet it was the Argentines who broke the deadlock after 20 minutes of play. A good team move eventually saw Martinez in a dangerous position and the forward beat Jefferson with a good volley.

Brazil responded in kind; Paulinho netted the equalizer six minutes later. The Argentina defense allowed the Corinthians midfielder too much space after a Neymar free kick, and he headed home from close range to make it 1-1.

The home side dominated play in the remainder of the game, but the fans had to wait until the dying minutes of the game for Brazil's second goal.

Leandro Desabato handled the ball inside his own area, leaving the referee no other choice but to award a spot kick. Neymar stepped up to take it and made no mistake from 12 yards.

The second leg will be on Oct. 3 at the Bicentenario stadium in Resistencia City.

Follow GOAL.COM USA on

Brazil

1
Jefferson
Goalkeeper
3.5
-
Lucas
Defender
-
-
Dedé
Defender
2.5
-
Réver
Defender
3.0
6
Fábio Santos
Defender
-
20
Jadson
Midfielder
62′
2.0
8
Paulinho
Midfielder
26′ 80′
3.5
5
Ralf
Midfielder
2.0
37
Lucas
Midfielder
76′
3.0
11
Neymar
Striker
26′ 88′ 94′
3.0
-
Luis Fabiano
Striker
68′
2.5

Argentina

2.5
1
Óscar Ustari
Goalkeeper
3.5
3
1.5
2
-
27
G. Peruzzi
Defender
3.5
2
Lisandro López
Defender
73′
3.0
6
2.0
11
Maxi Rodríguez
Midfielder
3.0
5
Guiñazu
Midfielder
3.0
22
Rodrigo Braña
Midfielder
3.5
-
4.5
-

Substitutes

10
Thiago Neves
Midfielder
62′
2.5
-
Wellington Nem
Midfielder
76′
2.5
9
2.5

Substitutes

-
18
-
9
-
-

Coach/Manager

-
3.5

Coach/Manager

3.5
-
 
  • Goal
  • Own Goal
  • Penalty
  • Penalty Missed
  • Yellow Card
  • Assist
  • Penalty Save
  • Penalty Shootout Goal
  • Penalty Shootout Miss
  • Yellow Card / Red Card
  • Red Card
  • Substitution IN
  • Substitution OUT
  • Injury
  • Goal.com Rating
  • Goal.com Man of the Match
  • Goal.com Flop of the Match
  • Top & Flop Global Ranking
  • Fans' Man of the Match
  • Fans' Flop of the Match
Post a new comment
4 Comments
Pernel AdonisLess than a minute ago
Neymar Player of the match not the flop of the match, he gave the assist for the first goal, and scored the winner goal
-1
Conner WaldenLess than a minute ago
Whatever. Argentina would've won if they had all of their best players. But since they're in the Champions League...
+1
Foysal Ahmed5 hours ago
.......
0
Mahmud Chowdhury6 hours ago
Ata ki Argentina Football team?