Rais Hamid Karzai alaani mauaji
17 Septemba, 2012 - Saa 07:26 GMT
Rais Hamid Karzai wa Afghanistan
amelaani vikali mauaji ya wanawake wanane katika shambulio la angani
lililotekelezwa na shirika la kujihami la nchi za Magharibi NATO.
Taarifa ya Bwana Karzai ilikuwa kali. Alishutumu
mauaji ya wanawake hao wanane yaliyotekelezwa na wanajeshi wanaoongozwa
na Serikali katika mkoa wa Laghman, ambako wanajeshi wa NATO wapo.Aliongezea kuwa ameteua kamati maalumu ya kuchunguza tukio hilo lililotendeka ili kuthibitisha kilichotokea.
Viongozi wa mkoa wanasema wanawake hao waliuawa walipokuwa wakikusanya kuni katika misitu eneo la milimani.
Msemaji wa vikosi vinavyoongozwa na NATO alituma risala zake za rambirambi. Ndege hiyo ya kijeshi ilikuwa imewalenga wapiganaji lakini huenda iliwaua raia kimakosa.
No comments:
Post a Comment