Mgomo wa walimu Chicago kuendelea
17 Septemba, 2012 - Saa 07:32 GMT
Vyama vya walimu mjini Chicago
nchini Marekani, vimeamua kuendelea na mgomo wao wa wiki moja kwa siku
zingine mbili wakati viongozi wao wakishauriana na wanachama takriban
elfu ishirini na moja kuhusu mkataba walioafikia na meya wa mji huo Rahm
Emanuel.
Mgomo huo wa walimu ni aibu kubwa kwa rais
Barack Obama,hasa kwa sababu unafanyika katika jimbo lake na pia
ikizingatiwa kuwa ni wakati wa kampeini za uchaguzi wa urais ambao na
yeye anagombea muhula wa pili.Meya wa mji huo, amekuwa akijaribu kufunga shule za kibinafsi na mahala pake kuweka shule za umma ambazo serikali inalipia na ambazo hazitazingatia sheria na kanuni nyingi, hatua ambayo inapingwa na walimu hao.
Meya huyo amesema kuwa sasa atataka ushauri wa mahakama ili kuharamisha mgomo huo.
No comments:
Post a Comment