Kijana Sterling kuichezea England
Mchezaji soka wa klabu ya Liverpool mwenye umri wa miaka 17,
Raheem Sterling, atashirikishwa katika kikosi cha England
ambacho kitapambana na Ukraine
katika mechi ya kufuzu ya Kombe la Dunia siku ya Jumanne.
Meneja Roy Hodgson pia amewachukua viungo wa kati Jake Livermore, mwenye
umri wa miaka 22, kutoka timu ya Tottenham, na Adam Lallana, mwenye umri wa
miaka 24, kutoka klabu ya Southampton.Mchezaji wa Arsenal, Theo Walcott, hataweza kucheza katika mechi hiyo, kwani anaumwa.
Walcott, pamoja na mchezaji wa Chelsea, Daniel Sturridge, hawakuweza kushiriki katika mazoezi ya timu ya taifa ya Jumatatu asubuhi.
Hata hivyo, Sturridge bado yumo katika kikosi hicho cha timu ya taifa.
Walinzi wa Chelsea, John Terry na Ashley Cole, pia hawatakuwepo katika mechi hiyo ya kundi H, kwani wote wana majeraha ya vifundo vya miguu.
Hodgson alielezea kwamba Walcott anaugua homa, na amerudi katika klabu yake, lakini kuna matumaini Sturridge aliyekuwa na maumivu ya tumbo huenda akawa amepona.
Nahodha Steven Gerrard ameelezea kufurahishwa na hatua ya Sterling kushirikishwa katika timu ya taifa, ambaye msimu huu mara mbili alikuwa kati ya wachezaji 11 wa kwanza kuingia uwanjani katika mechi mbili, na mwishoni mwa msimu uliopita alishirikishwa katika mechi tatu kama mchezaji wa zamu.
“Nadhani
anastahili kukaribishwa katika mwito huu. Tofauti aliyoileta kimchezo ni ya
kusisimua,” alielezea Gerrard.
"Yeye ni kati ya mwanga wetu unaomulika mno. Muhimu ni kwamba yeye
hucheza kwa utulivu. Nadhani haitachukua muda mrefu ubunifu wake kujitokeza
kikamilifu."
No comments:
Post a Comment